JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA WIKI YA UKAGUZI WA...
Shabaha kuu ni kuhamasisha wadau wa elimu kuhusu umuhimu wa ukaguzi wa shule katika azma ya kuinua ubora wa elimu nchini i...
of 2

Press ralease ukaguzi wa shule

Press ralease
Published on: Mar 4, 2016
Published in: Education      
Source: www.slideshare.net


Transcripts - Press ralease ukaguzi wa shule

  • 1. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAARIFA KWA UMMA MAADHIMISHO YA WIKI YA UKAGUZI WA SHULE Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaadhimisha Wiki Ya Ukaguzi Wa Shule mwaka huu kuanzia tarehe 8/9/2014 hadi tarehe 12/9/2014 ambapo maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi kitaifa jijini Dar es Salaam katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Dar es Salaam University College of Eduacation - DUCE) na kuendelea kwa shughuli mbalimbali za kukagua shule nchi nzima. Maadhimisho ya Wiki ya Ukaguzi wa Shule yanalenga kutangaza shughuli za Wakaguzi wa Shule kwa wadau wote wa elimu kwa kutumia njia mbali mbali zikiwemo Magazeti, Redio, Televisheni, Makongamano na kuwashirikisha Viongozi wa Elimu na Serikali katika zoezi zima la kukagua shule ili kuamsha ari ya kufanya kazi kwa pamoja zaidi na kushirikiana. Majukumu ya Wakaguzi wa Shule ni pamoja na Kukagua shule ili kuhakikisha utoaji bora wa taaluma na uendeshaji fanisi wa shule; Kutoa ushauri kwa wadau wa elimu kuhusu njia bora za ufundishaji na ujifunzaji; Kutoa ushauri kuhusu uanzishwaji/usajili wa shule mpya; Kuchochea maendeleo na mabadiliko katika elimu kwa kufanya utafiti wa kielimu; na kuandika makala mbali mbali, kuwaimarisha walimu katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo ya shule kwa kutoa ushauri wa kitaalam na kitaaluma.
  • 2. Shabaha kuu ni kuhamasisha wadau wa elimu kuhusu umuhimu wa ukaguzi wa shule katika azma ya kuinua ubora wa elimu nchini ili kufanikisha Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta ya Elimu. Shughuli zitakazofanyika katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukaguzi wa Shule ni pamoja na Kongamano litakalowahusisha Wataalam mbalimbali wa elimu ambapo kutakuwa na makala zitakazowasilishwa kuhusu Ukaguzi wa Shule na majadiliano yatafanyika. Kongamano hilo litafanyika siku ya ufunguzi wa maadhimisho hayo tarehe 8/9/2014 katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam. Shughuli nyingine zitakazofanyika nchi nzima katika wiki hiyo ni Kukagua shule kwa kuwashirikisha viongozi wa elimu na serikali na kufanya tathmini ya ukaguzi wa shule katika kila ngazi na hatimaye kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha ukaguzi katika sekta ya elimu nchini. Washiriki wa maadhimisho ya Wiki ya Ukaguzi wa Shule ni wadau wote wa elimu wakiwemo wazazi, walezi, walimu, wanafunzi, watendaji, wasimamizi na Viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu; na Vyuo Vikuu vya hapa nchini; Wakaguzi wa Shule ngazi ya Kanda na Wilaya. Washiriki wengine ni pamoja na Viongozi wa Taasisi zisizokuwa za kiserikali zikiwemo TEN/MET, TWAWEZA, CWT, TAMONGSCO, TAHOSSA, na Wawakilishi wa Wakuu wa Vyuo vya Ualimu na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi. “UKAGUZI FANISI NA ENDELEVU KWA ELIMU BORA” Katibu Mkuu WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 01/09/2014